Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1005 | 1006 | (Page 1007) | 1008 | 1009 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
  Ni kipindi cha mwisho kabla ya uchaguzi, na washiriki wengi walishiriki kutoa mchango wao kuhusu mchakato ulivyokuwa, na neno ama wosia wao kwa waTanzania wote
  KARIBU

  0 0

   Mwandishi Wetu, Geita
  MGODI wa dhahabu wa geita (GGM), umezalisha ajira zaidi ya 200 kwa jamii baada kuwekeza zaidi ya Sh1.7 Bilioni kupitia programu ya Uchumi na Maendeleo (GEDP) ambayo imelenga kusaidia wakulima na wajasiriamali wadogo na wa kati, wanaoishi jirani na mgodi.


  Akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Geita, Fatma Mwassa alipotembelea mgodini hapo juzi, Makamu wa Rais wa Anglo Gold Ashanti/GGM, Simon Shayo alisema mpango umelenga kubadili hali za maisha ya wakazi kuwa tofauti na ilivyokuwa kabla mgodi haujaanza kufanyakazi.


  Alisema mradi umewasaidia wakazi hao na familia zao kuwa na fani ambazo wanazitumia kwa uzalishaji na mbinu za kujipatia masoko katika mji wa Geita na maeneo mengine nje ya mgodi huo.


  "Hiyo inatokana na ubora wa mafunzo ambayo tunawapa sanjari na mbinu za biashara" alisema meneja huyo na kuongeza kuwa zaidi ya ekari 800 zimetengwa kwa ajili ya kilimo cha Alizeti, Mpunga na mazao mengine na utafiti wa udongo umekamilika.


  Pia utengenezaji wa miundombinu kwa ajili ya umwagiliaji unafanyika na upande mwingine, ununuzi wa mashine za umwagiliaji, uchomeaji, mashine za kuzalisha umeme, vyerehani na mashine za kudarizi kwa ajili ya wananchi hao wa Geita vinafanyika.


  Meneja huyo alibainisha kuwa lengo ni kuhakikisha kunakuwa na mnyororo endelevu wa thamani ya mazao ya kilimo kwa kuongeza viwango vyao vya ufahamu katika mfumo wa masoko na kuongeza ubora wa mazao na wigo wa biashara kwa wajasiriamali hao wadogo na kati.


  "Tunatumia programu hiyo kwa ajili ya kuwawezesha wakazi iuchumi na pia kupunguza kiwango cha umaskini" anasema na kuongeza kuwa mpango huo utapunguza idadi ya vijana wasio na ajira Geita na wengine ambao wamekuwa wakijitumbukiza katka uhalifu mgodini.


  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Fatma Mwassa alisema kuna matumaini makubwa kuwa jitihada hizo za GGM zitazidi kukua na kubadili maisha ya walio wengi kwa kuwawezesha kiuchumi wananchi wa Geita.


  "Naamini sasa watauza mazao na bidhaa zilizokamilika na sio ghafi kama awali na sio kwa Geita pekee bali pia nchi jirani" alisema Mwassa. Kulingana na takwimu za hivi karibuni, kilimo kimetoa ajira kwa asilimia 88 ya watanzania nchini.

  0 0

  BJ and Hellen Mwakyoma (Gwantwa) Wa Chicago-IL anasikitika kutangaza kifo cha Mama yao Mama  Tamali Mwakyoma, Kilichotokea nchini India juzi October 17, 2015 alikokwenda kwa matibabu. Habari ziwafikie Ndugu jamaaa na Marafiki Popote Pale walipo.

  BJ na Hellen wanatarajia kuondoka Marekani Jumanne kurudi Tanzania kwa Mazishi, ambapo shughuli za awali za msiba ziko nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es salaam, nyuma ya jengo la Kamisheni ya Vyuo Vikuu barabara ya Rose Garden. 

  Kwa pole na salaam za rambi rambi 
  mnaweza kuwasiliana na Gwantwa @ 773-262-2703

  Bwana ametwaa, na Bwana Ametoa, 
  Jina la Bwana na Lihimidiwe.
  AMINA

  0 0

  Sehemu ya wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya TAS iliyoko Arusha wakati wa
  0 0


  0 0


   Meza kuu ikitambulishwa  katika mahafali ya 14 ya Kidato cha Nne ya Tanzania Adventist Secondary School iliyoko  Arusha,  Jumapili iliyopita.
    Mgeni rasmi Brigedia Jenerali George Mshamba akitoa nasaha katika mahafali ya 14 ya Kidato cha Nne ya Tanzania Adventist Secondary School iliyoko  Arusha,  Jumapili iliyopita.

   Wahitimu wa Kidato cha Nne wa Tanzania Adventist Secondary School iliyoko  Arusha  katika mahafali ya 14 ya shule hiyo yaliyofana sanja Jumapili iliyopita. Wa kwanza kushoto na wa tatu ni waalimu wao
  Wahitimu wa Kidato cha Nne wa Tanzania Adventist Secondary School iliyoko Usa River, Arusha,  katika mahafali ya 14 ya shule hiyo yaliyofana sana Jumapili iliyopita. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Meneja wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Bw. Calvin Martin (wa pili kushoto), akiwaonyesha Watafiti kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojkia na wageni kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea, mitambo mipya ya kuzalisha bia, walipotembelea kiwanda hicho, Dar es Salaam jana kujifunza kuhusu uendeshaji na aina ya mitambo.
   Maofisa kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wageni wao kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea wakimsikiliza kwa makini, Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw Calvin Martin )wa pili kulia), walipofika kiwandani hapo Dar es Salaam jana kujifunza kuhusu uendeshaji wa kiwanda, aina ya mitambo na ushirikiano na taasisi zingine. Kulia ni Meneja Usalama wa TBL, Bw. Renatus Nyanda.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  IMG_9022
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga (katikati) wakimkaribisha mmoja wa wageni waalikwa katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

  Na Mwandishi wetu, Zanzibar
  SERIKALI ya mapinduzi Zanzibar imesema kuwa itaendelea kuthamini fursa mbali mbali zinazotolewa na Umoja wa Mataifa (UN) ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote bila ya ubaguzi.

  Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman wakati akihutubia katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar, alisema umoja huo umekuwa sekta muhimu ya kuunga mkono juhudi za maendeleo ya serikali katika sekta mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

  Alisema kuwa Zanzibar ikiwa miongozi mwa nchi zinazoendelea barani Afrika inaendelea kutumia vizuri fursa zinazotolewa na umoja huo kwa lengo la kujenga jamii bora zenye kipato na uwezo wa kati kwa lengo la kupunguza umasikini nchini.

  Waziri Haroun alifahamisha kuwa miradi mbali mbali ya maendeleo inayotolewa na umoja huo imekuwa nyenzo muhimu ya kuisaidia serikali kuhudumia wananchi wake kwa ufanisi zaidi.

  Alisema kutokana na misaada hiyo Zanzibar pia imekuwa mdau muhimu wa umoja huo kwani ni miongoni mwa nchi yenye urithi wa kimataifa kupitia maeneo ya Mji Mkongwe jambo ambalo ni ishara tosha ya mahusiano mema kati ya umoja huo na serikali.
  IMG_9075
  Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar wakibadilishana mawazo wakati wa kuwasili kwa wageni waalikwa kwenye sherehe hizo.
  “ Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajali kwa kiasi kikubwa juhudi za Umoja wa Mataifa kwa kutuunga mkono, nasi tunaendelea kutumia vizuri miradi mnayotuunga mkono.

  Pia tunaendelea kukuombeni mtusaidie pale tutakapohitaji msaada wenu kwa Nyanja tofauti kwani bajeti ya serikali haitoshi kukidhi mahitaji yote ya kuendesha serikali.”, Alisema Waziri Haroun.

  Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alikiri kuridhishwa kwake na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya umoja huo na kuahidi kuendelea kushirikiana vizuri na serikali ili kufikia dhana ya maendeleo endelevu Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.

  Bw. Rodriguez alibainisha kuwa umoja huo bado unaendelea kufanya tathimini na utafti juu ya masuala mbali ya kisiasa na kijamii nchini ili kuona ni kwa jinsi gani watasaidia kuunga mkono maeneo hayo kwa maendeleo ya nchi.

  0 0

   
  Kiongozi wa familia hiyo, Albert Michael, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geita.

  Na Rashid Zahor, Geita.
  FAMILIA ya mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli imesema Watanzania watakuwa na bahati ya kumpata kiongozi mchapakazi, mwenye msimamo na anayependa maendeleo.

  Imesema iwapo Dk. Magufuli atachaguliwa kuwa rais, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii, atawaletea maendeleo makubwa kwa kuwa ni mtu mwenye msimamo, asiyeyumba na anayependa maendeleo.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na kiongozi wa familia hiyo, Albert Michael, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geita.

  Mzee Albert hakuwepo Katoma juzi wakati msafara wa Dk. Magufuli uliposimama kwa muda nyumbani kwa babu yake, ambako alipata nafasi ya kuzuru kaburi lake na la bibi yake mzaa wa baba na kuwaombea dua.

  "Watanzania wasiwe na wasiwasi, Magufuli ni mtu anayependa watu na maendeleo na ni mchapakazi,"alisema Mzee Albert, alipokuwa akijibu swali kuhusu sifa za mgombea huyo tangu alipokuwa mtoto.

  Aidha, Mzee Albert alisema Dk. Magufuli si mpole, sio mkali sana, lakini ni mtu mwenye msimamo na asiyeyumba katika jambo analotaka kulifanya.
  Mzee Albert, ambaye ndiye aliyeachiwa mji wa Katoma kwa sasa, liliko chimbuko la ukoo wa Dk Magufuli, akiwa miongoni mwa wadogo zake marehemu baba mzazi wa mgombea huyo, alisema familia yao ipo pamoja naye na inamuombea Mungu aweze kutimiza dhamira yake ya kuwa rais wa awamu ya tano ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  "Ninachowahakikishia Watanzania ni kwamba Oktoba 25, watampata kiongozi bora, asiye na ubaguzi wa aina yoyote,"'alisema mzee huyo.
  Akizungumzia majina ya mgombea huyo, alisema jina la Pombe alipewa na bibi yake siku alipozaliwa, kwa kuwa siku hiyo alikuwa akipika pombe. 

  Alisema jina la Magufuli lilitokana na kupenda kwake michezo.
  "Siku John alipozaliwa, bibi yake alipopelekewa taarifa, alisema 'huyo mume ni mume wangu aitwe pombe'," alisema mzee huyo, ambaye alifika Geita juzi usiku akitokea Chato.

  Juzi, Dk. Magufuli alitembelea kwenye makaburi ya babu na bibi yake mzaa wa baba, eneo la Katoma, wilayani Geita Vijijini na kufanya ibada ndogo ya kuwaombea dua.

  Dk. Magufuli alifika nyumbani kwa babu yake saa 6.30 mchana na kupokewa na baba yake mdogo, Sylvestr Magufuli, kabla ya kupelekwa kwenye makaburi hayo, ambako aliongoza ibada ndogo ya kuwaombea dua.
  Akizungumza kwenye eneo hilo, baba huyo alisema makaburi hayo ni ya babu na bibi wa mgombea huyo pamoja na ndugu zake wengine, waliofariki dunia miaka mingi iliyopita.

  Alisema asili ya ukoo wa Dk. Magufuli ni Katoma, ambako ndiko baba yake alikozaliwa kabla ya kuhamishia makazi yake Chato.

  "Tumezoea kumuona ndugu yetu kwenye tv na kumsikiliza kwenye redio, leo tumefurahi kumuona yeye mwenyewe,"alisema na kuongeza kuwa wanamuombea dua kwa Mungu ili aweze kuchaguliwa kuwa rais.

  Kwa upande wake, Dk. Magufuli alisema alifarijika kufika tena katika eneo hilo kwa sababu ndiko alikozaliwa na kukulia na pia ndiko ukoo wake ulikoanzia.
  Kusoma zaidi bofya HAPA.

  0 0  0 0

  Na January Makamba

  Tarehe 25 mwezi huu Oktoba, Watanzania watapiga kura kumchagua rais wao wa tano, wabunge na madiwani. 
  Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu umekuwa na msisimko mkubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa mfumo wa siasa za vyama vingi mwaka 1995. Mengi yamendikwa kuhusu uchaguzi huu, hususan kutokana na hisia kwamba safari hii Upinzani una nafasi ya kukiondoa madarakani moja ya vyama vikubwa na vyenye muundo bora barani Afrika, chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM). Matukio mbalimbali kuelekea uchaguzi huo yameleta shauku inayoweza kutengeneza hadithi ya kusisimua. 
  Nikiwa sehemu ya Timu ya Kampeni ya CCM,na kwa manufaa ya wote ambao wangependa kuwa na mtizamo tofauti, ninatoa sababu 9 kwa nini tunaamini kuwa CCM itaibuka mshindi na kwanini Dkt John Pombe Magufuli atakuwa Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

    Majimbo kumi ya kufa au kupona kati ya CCM na CHADEMA. Masha akamatwa tena.Yote haya utayapata katika magazeti ya leo;  https://youtu.be/he5sNUP8L1A
   
  Magufuli kutikisa Dar kwa siku tatu. NEC yasema kukusanyika mita 200 ni hujuma na kwamba kutazua hofu kwa wapiga kura; https://youtu.be/1cf2IYpQLjU

  Mchungaji afungwa kifungo cha maisha kwa kumbaka mwanae. Wataalam wasema ni vigumu chopa kulipuka ;  https://youtu.be/XPE-WhIy80E

  Simba ,Yanga vitani leo, Kiiza mchezaji bora September. MO yaitaka Simba kwa Bil.20. Pata habari za michezo katika magazeti ;  https://youtu.be/DdCCFWuu-ow

   Mbowe anena mazito katika mazishi  wa Dr.Makaidi.Pata habari kutoka magazetini zilizopewa kipaumbele kwa siku ya leo;https://youtu.be/JgWToCo-FNo


  0 0

  MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imemuhukumu kifungo cha maisha jela Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Athanas Ngomai (30), baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 15.


  Pia, mahakama hiyo imetaka mchungaji huyo amlipe fidia ya Shilingi  milioni 2 mlalamikaji ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mbondole iliyoko Ukonga. 

  Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, Ngomai alianza kumbaka mtoto huyo akiwa na umri wa miaka kumi na moja, wakati huo akisoma darasa la tatu.

  Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Ilala, Saidi Mkasiwa alisema Mahakama imemtia hatiani mchungaji huyo baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watano uliotolewa mahakamani hapo akiwamo daktari.

  Alisema kutokana na ushahidi huo, upande wa mashtaka ulithibitisha shitaka hilo pasi kuacha shaka, hivyo anamtia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wake. “Mahakama yangu inakutia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wako, utatumikia kifungo cha maisha jela ili liwe fundisho kwa wazazi wengine wenye tabia mbaya kama yako, pia unatakiwa kumlipa fidia mlalamikaji ya Sh2 milioni,” alisema.

  Kabla ya hukumu kutolewa, Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa kwani alitakiwa kuwa mfano bora kwa jamii.

  Hata hivyo, mahakama ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea.
  Mchungaji huyo aliiomba mahakama itende haki kwani yeye hajui sheria na kosa hilo limetengenezwa halina ukweli wowote.

  Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa mahakamani hapo, mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya Januari 21, mwaka 2008 katika eneo la Mbondole, Ukonga wilayani Ilala, Dar es Salaam.
  Ilidaiwa kuwa mshitakiwa huyo alianza kumbaka mtoto wake huyo akiwa na miaka kumi na moja.

  0 0

  Mbwa 
  Watafiti wanakubaliana mbwa wamekuwa wakitumiwa na binadamu kwa miaka 15,000,Utafiti mpya unaonyesha kuwa Mbwa walianza kufugwa kwa mara ya kwanza katikati mwa bara Asia.


  Watafiti hao walichunguza chembe za msambojeni (DNA) za aina 165 ya mbwa, kutoka mataifa 38 katika kile wanachosema ni utafiti mkubwa zaidi, kuwahi kufanyika duniani kuhusiana na uzao wa mbwa.

  Utafiti huo unasema kuwa Nepal na Mongolia ni maeneo ya kwanza kabisa ambapo mbweha walianza kuwa marafiki wakubwa wa binadamu, lakini haijasema ni lini tukio hilo lilifanyika.

  Kuna dhana nyingine kuwa mbwa walianza kufugwa kwa mara ya kwanza kusini mwa Uhina, bara ulaya, Siberia, au Mashariki ya Kati, yapata miaka elfu kumi na mitano iliyopita.

  Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa kwenye toleo la hivi punde la jarida la Proceedings of the National Academy of Sciences, linalochapishwa nchini Marekani. 

  0 0

  Wanafunzi wakiwa katika pozi na vyeti pamoja na vikombe walivyo zawadiwa.

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
  WALIMU na viongozi wa shule mbalimbali nchini wamekumbushwa kutoa elimu itakayowajengea uwezo wanafunzi kujitegemea mbali na elimu ya nadharia na vitendo darasani pekee.

  Rai hiyo imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa serikali, Bw. George Masaju alipokuwa akiongea wakati wa mahafali ya 8 na maadhimisho ya miaka 10 ya shule ya Patrick Mission High School jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

  Bw. Masaju ambae alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo ya kidato cha nne, alisema elimu hiyo ya kujitegemea itawasaidia vijana kujiamini na kupambana katika soko la ajira au kujiajiri wenyewe katika shughuli halali za kuwaingizia mapato.

  Alisisitiza pia umuhimu wa kuwafundisha vijana kukua katika mila, tamaduni na maadili bora ya kitanzania kwa ajili ya kudumisha uwepo wa ustawi katika taifa.

  “Wafundisheni vizuri historia ya nchi yetu na umuhimu wa kuwa wazalendo wa nchi hii,” alisema Bw. Masaju na kuongezakuwa ‘hakuna taifa lolote duniani lililowahi kuendelea na kuwa na nguvu kubwa kiuchumi na kiutawala ikiwa wananchi wake hawana uzalendo.’

  Awali katika taarifa ya shule hiyo ilielezwa kuwa hadi sasa, shule imeshasomesha wanafunzi 100 ambao ni yatima na kila darasa lina yatima wawili.

  Bw. Masaju aliipongeza shule hiyo kwa moyo wake wa kusomesha watoto yatima, kwani bila msaada huo, wasingepata elimu.

  Miongoni mwa watu aliowashukuru kwa kutoa msaada wa elimu kwa yatima ni Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais Jakaya Kikwete ambaye juhudi zake kupitia Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) pia amekuwa akisaidia shule hiyo.

  “Nawaomba watu wengine na taasisi mbalimbali ziendelee kuwasaidia ndugu zetu hawa,” alisema.

  Katika sherehe hizo, pia palikuwa na harambee kwa ajili ya kuwasaidia yatima kuweza kupata elimu.

  Akitoa ushauri kipindi hiki cha uchaguzi, alisema moja ya mambo yanayoweza kusaidia kutunza amani ya nchi ni kuzingatia katiba, sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza uchaguzi.

  “Hakuna jambo lolote la umma linalofanywa au kutekelezwa pasipo kuwekewa taratibu za kisheria,” alifafanua.

  Alisema ndio maana kutokana na masharti ya sheria mbalimbali, wananchi baada ya kupiga kura wanapaswa kurejea katika makazi yao kusubiria matokeo yatakavyokuwa yanatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kupitia wasimamizi wa uchaguzi au na Tume yenyewe kwa matokeo ya uchaguzi wa Rais.

  Sheria ya Taifa ya Uchaguzi inakataza katika kifungu chake cha 104 kufanyika kwa mikutano au mikusanyiko siku ya uchaguzi au kufanya mikutano ndani ya umbali wa mita 200 kutoka katika kituo cha kupigia na kuhesabia kura.

  Alitumia nafasi hiyo pia kutoa wito kwa viongozi wa dini kuwashauri waumini wao kuitii serikali inapokuwa inatekeleza jukumu lake la kusimamia amani, usalama na utengamano katika nchi.

  Mmoja wa wazazi katika hafla hiyo, Bw. Ezekiel Marwa aliwataka watoto waliohitimu kutojiingiza katika makundi ya madawa ya kulevya na ulevi.

  0 0

  ????????????????????????????????????Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Rehani Athumani wa NHIF (katikati), akizungumza na wanachama wapya wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kupitia Mpango wa KIKOA (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango huo kuwakabidhi kadi ya uanachama wapatao 25 wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kupitia Mpango mpango wa KIKOA (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi YETU MICROFINANCE PLC, Bw.Altemius Millinga, (watatu kulia) Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Bw. Eugen Mikongoti. hafla hiyo ilifanyika Yombo Dovya Oktoba 20, 2015 Jijini Da es Salaam.
  ????????????????????????????????????Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya YETU MICROFINANCE PLC, Bw.Altemius Millinga (kushoto), akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo.
  ????????????????????????????????????
  Wanachama wapya wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kupitia Mpango wa KIKOA wakifuatilia mada mbalimbali wakati hafla hiyo.

  0 0

  Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Asubuhi Hii October 21, 2015.

  SIMUtv: Tanzania imetajwa kutofanya vizuri katika utoaji wa huduma kwa wazee katika Nyanja mbalimbali hususani Afya na Mazingira. https://youtu.be/cnYXI1-elnI

  SIMUtv: Rais Jakaya Kikwete ameliagiza Jeshi la Polisi nchi kufanya kazi  kwa weledi ili kuhakikisha Taifa linamaliza uchaguzi Mkuu wa Amani na utulivu https://youtu.be/ktVuerobzYY

  SIMUtv: Mgombea Urais CCM Dkt. John Magufuli awaondoa hofu wakulima wa zao la Pamba na kuahidi kuongeza bei ya zao hilo kwa wanunuzi. https://youtu.be/L2PB7R2F41c

  SIMUtv: Serikali visiwani Zanzibar Imeyakaribisha makampuni toka mataifa Mbalimbali kuwekeza mitaji katika mji wa Fumba ili kutoa fursa za ajira kwa Vijana https://youtu.be/CJSDknBLDHk

  SIMUtv: Mamlaka Ya chakula na Dawa TFDA kanda ya ziwa imeharibu bidhaa bandia za Pombe aina ya Viroba zenye thamani ya zaidi ya Mil. 80. https://youtu.be/rwz7ek0zWNk

  SIMUtv: Mkuu wa wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora awataka wakazi wa wilaya hiyo wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa Kuwa Hali ya ulinzi imeimarika. https://youtu.be/sOIK46Lp-3E

  SIMUtv: Ligi kuu Tanzania bara yasimamishwa kwa muda na kupisha maandalizi ya timu ya taifa katika michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia;  https://youtu.be/hkGFA9Hs-e0

  SIMUtv: Nyota wa kimataifa wa timu ya taifa ya Nigeria Emanuel Eminike atangaza rasmi kustaafu kuchezea timu hiyo;https://youtu.be/UMYdQynkcbQ

  SIMUtv: Wakazi wa kijiji cha bendera wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Wameombwa kuweka kando tofauti zao za kisiasa katika kujadili mgogoro wa Mpaka. https://youtu.be/vepp3pVgclU


  0 0


  0 0

  Hapa ni katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga ambako jana Jumanne,Oktoba 20,2015,wadau mbalimbali wa amani mkoani Shinyanga wamekutana kwa ajili ya majadiliano ya ushirikiano wa kudumisha amani katika kipindi cha uchaguzi mkuu 2015.Kikao hicho kimeandaliwa na uongozi wa mkoa wa Shinyanga likiwemo jeshi la polisi kwa kushirikiana na Shirika la Save The Children linalojihusisha na utetezi wa haki za watoto.

  Mambo kadha wa kadha yamejadiliwa ikiwemo kuhakikisha ulinzi na usalama wa watoto kabla,wakati na baada ya uchaguzi,lakini pia viongozi wa vyama vya siasa,wagombea na wanachama kuheshimu na kutekeleza sheria,kanuni,maadili na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi pamoja na sheria nyinginezo za nchi katika kipindi chote cha uchaguzi.
  Mgeni rasmi katika kikao hicho alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa. Fuatilia matukio katika picha hapa chini-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akifungua kikao hicho cha wadau ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa serikali haiko tayari kuona amani ya nchi inavurugwa hivyo itachukua hatua kali za kisheria kwa watu wote watakaofanya vurugu siku ya uchaguzi.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  KATIKA kuhakikisha wateja wake kutokuwa nyuma kiteknolojia na kupata huduma bora za mawasiliano ya kisasa kwa kutumia mtandao wa intanet,kampuni ya Vodacom Tanzania imezindua simu mpya ya Smart 6 ya gharama nafuu ambayo wananchi wengi wanaweza kumudu kuinunua.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa simu hii Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Kelvin Twissa amesema kuwa simu hii  imelenga wateja wake wenye vipato vya kawaida ili kuwawezesha kufurahia huduma za kisasa za matumizi ya simu za mkononi za Smartphone ili waweze kwenenda na teknolojia.

  “Vodacom siku zote tumekuwa tukiwasikiliza wateja wetu na ndio maana tumeingiza sokoni simu hii ili kuwawezesha kufurahia matumizi ya simu za kisasa za smart ambazo zinawawezesha kupata huduma za internet na program nyinginezo za kurahisisha maisha yao na kuwa murua ikiwemo kupiga picha wazipendazo kwa kutumia simu zao,”Alisema Twissa.

  Aliongeza kuwa simu hii ya Smart 6 ambayo itakuwa inauzwa kwa bei nafuu kabisa ya shilingi 90,000/- ina kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi,ina kamera ya kisasa,uwezo zaidi wa kuperuzi intanet ya 3G, nafasi kubwa ya kuweka kumbukumbu na inakaa na betri kwa muda mrefu. Hii ni simu ya kipekee ambayo kila mteja anatakiwa kuwa nayo.

  Alisema simu hizi zinapatikana katika maduka yote ya Vodacom na katika matamasha yote yanayofanywa na kampuni yetu nchi nzima ya Vodacom tumekufikia.Mteja yeyote atakayenunua simu hii atajipatia ofa kabambe kabisa ya kupata 500MB bure na uwezo wa kutuma jumbe fupi za maneno zipatazo 200 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 6 bure.

  Aliwataka wateja wa Vodacom na wananchi wengine kwa ujumla kuchangamkia fursa hii na kukamata Smart 6 kwa gharama nafuu ili kuendelea kupata taarifa za huduma mbalimbali zinazopatikana kwa kuperuzi mtandao wa intanet.Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu www.vodacom.co.tz au kurasa zetu za Facebook na Twitter.
   Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(kushoto)akiwanesha  waandishi wa habari(hawapo pichani) simu mpya aina ya Smart 6 wakati wa uzinduzi wa simu hiyo yenye kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi na ina kamera ya kisasa na uwezo zaidi wa kuperuzi intanet ya 3G,itapatikana kwa bei nafuu kabisa shilingi 90,000/- inapatikana katika maduka yote ya kampuni hiyo.Mteja yeyote atakayenunua simu hiyo atajipatia ofa kabambe kabisa ya kupata 500MB bure na uwezo wa kutuma jumbe fupi za maneno zipatazo 200 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 6 bure.Kulia ni Mkuu wa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo,Samson Mwongela.
   Mkuu wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Mwongela(kulia)akimshuhudia Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(kushoto)akiwanesha  waandishi wa habari(hawapo pichani) simu mpya aina ya Smart 6 wakati wa uzinduzi wa simu hiyo yenye kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi na yenye kamera ya kisasa na uwezo zaidi wa kuperuzi intanet ya 3G, itapatikana kwa bei nafuu kabisa shilingi 90,000/- inapatikana katika maduka yote ya kampuni hiyo.Mteja yeyote atakayenunua simu hiyo atajipatia ofa kabambe kabisa ya kupata 500MB bure na uwezo wa kutuma jumbe fupi za maneno zipatazo 200 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 6 bure.
   Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(kushoto) pamoja na Mkuu wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Mwongela,wakijipiga selfiii kwa kutumia simu mpya aina ya Smart 6 waliyoizindua leo yenye kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi na yenye kamera ya kisasa na uwezo zaidi wa kuperuzi intanet ya 3G, itapatikana kwa bei nafuu kabisa shilingi 90,000/- katika maduka yote ya kampuni hiyo.Mteja yeyote atakayenunua simu hiyo atajipatia ofa kabambe kabisa ya kupata 500MB bure na uwezo wa kutuma jumbe fupi za maneno zipatazo 200 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 6 bure.

  Vodacom launches the affordable Smart 6 phone
  In ensuring that their customers stay connected to the latest  technology, and that they get the best services and communications using Internet, Vodacom Tanzania has introduced yet another smartphone; the Smart 6 which is the most affordale smartphone .

  Speaking during the launch, Vodacom  Tanzania’s Head  of Marketing and Communication,Kelvin Twissa said the phone price is Tshs 90,000 and will enable many customers  to enjoy the modern amenities of the  Smart phone and keep up with technology.

  “The Smart 6 is the latest Vodacom device to launch in Tanzania with the express purpose of making the cost to connect more affordable,” said Twissa.
  The Smart 6 comes with the latest Android application, features a 4-inch WVGA display for better viewing experience, 4GB internal storage, 1GHz dual-core processor and can support internet speeds of upto 21mbps.With a Longer Battery Life and at a price that most citizens can afford, this is everyones smartphone.

  Additionaly, customers get 500MB and 200 free text messages for a period of 6 months. The device will be available in our Vodacom shops and authorized dealers and promoters countrywide.
  For more details visit our website www.vodacom.co.tz or follow us on Facebook/Twitter .

older | 1 | .... | 1005 | 1006 | (Page 1007) | 1008 | 1009 | .... | 3272 | newer