Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

IDADI YA WAPIGA KURA KIMKOA, KIJINSIA NA KIUMRI


MAHAFALI YA 14 YA KIDATO CHA NNE MKOLANI SEKONDARI JIJINI MWANZA YAFANA.

0
0
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza Mwl.Asensio Mathias (Mwenye Kinasa Sauti) akizungumza katika Mahafali ya 14 ya Kidato cha Nne katika shule hiyo yaliyofantika jana Octoba16,2015 katika Ukumbi wa Shule hiyo.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 14 ya kidato cha Nne Mkolani Sekondari ya Jijini Mwanza Ndg.Bituro Kazeri (Wa tatu kila upande) ambae ni Afisa Habari wa Taasisi ya Sayansi ya Jamii TASAJA akijiandaa kuwakabidhi vyeti wahitimu wa shule hiyo katika Mahafali yaliyofanyika jana shuleni hapo
Mwonekano ndani ya Ukumbi.

NISHATI YA JOTOARDHI KUIPANDISHA HADHI HIFADHI YA WANYAMAPORI SELOUS

0
0
 Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo ya Biashara, Mhandisi Kato Kabaka (aliyesimama) kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania, akitoa elimu ya nishati ya Jotoardhi kwa wafanyakazi wa hifadhi ya wanyamapori Selous na jinsi gani nishati hiyo itaongeza idadi ya watalii.
 Wafanyakazi wa hifadhi ya wanyamapori Selous na kampuni ya uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania wakimsikiliza kwa makini Mhandisi Kato Kabaka (hayuko pichani) alipokuwa akiwaelimisha namna nishati ya Jotoardhi itakavyoongeza idadi ya watalii kupitia mabwawa ya kuogelea ya maji moto yatakayojengwa ndani ya hifadhi hiyo.

Bwana Eneck Majahasi (aliyesimama) akihitaji ufafanuzi ikiwa mitambo ya uzalishaji wa nishati ya Jotoardhi itakayojengwa ndani ya hifadhi ya Selous haitakuwa na madhara kwa wanyamapori walioko ndani ya hifadhi.

Na. Lilian Lundo - Maelezo

Kuendelezwa kwa nishati ya Jotoardhi Tanzania itaipelekea kupanda hadhi kwa hifadhi ya wanyamapori Selous.


Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo ya Biashara, Mhandisi Kato Kabaka kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania wakati akizungumza na wafanyakazi wa hifadhi ya wanyamapori Selous, kambi ya Matambwe alipokuwa akitoa elimu ya nishati ya Jotoardhi yenye viashiria (majimoto) ndani ya hifadhi hiyo, leo.


“Kama utafiti utaonyesha chanzo cha nishati ya Jotoardhi kipo ndani ya hifadhi, basi nishati hiyo itapelekea hifadhi ya Selous kuongeza idadi ya watalii kwa kujenga mabwawa ya kuogelea yatakayokuwa na maji ya moto na kujenga vibwawa vidogo ndani ya vibanda vya kupumzikia kwa ajili ya kuweka miguu wageni watakao kuwa wakitembelea hifadhi hiyo.” Alisema Mkurugenzi Kato.


MKUTANO WA WAKUU WA TEHAMA - RADIO ONE

0
0
Baada ya kumalizika kwa mkutano wa Viongozi TEHAMA Nchini Kenya Vyombo kadhaa vya habari vimepata Kunihoji ikiwa ni pamoja na Radio One - Kupitia African Panorama.
Ambapo nimetolea ufafanuzi wa key take a ways kwenye mkutano na hasa kubobea kwenye eneo langu la utaalam ambapo ndio mijadala niliyo jadili - Usalama mitandao.

SERIKALI KULIPA MADENI YA WATUMISHI WA SERIKALI ZA MITAA.

0
0

Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (wa pili kutoka kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu namna Serikali  inavyoshughulikia madai ya watumishi walio katika Serikali za Mitaa wasio walimu. 

Na Magreth   Kinabo-maelezo
SERIKALI  imetenga  kiasi cha fedha cha  Sh. bilioni tano ( 5.93) ikiwa ni madeni ya mishahara ya  Watumishi wa Mamlaka za Serikali za  Mitaa(TALGWU) na  Sh. bilioni nne(4) kwa ajili ya kulipa madeni  ya yasiyohusu mishahara, fedha ambazo zitalipwa Oktoba mwaka huu.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa leo na  Kaimu  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB  Mkwizu  wakati akizungumza  na waandishi wa habari kuhusu  madai na madeni  ya watumishi hao  kwenye  ukumbi  wa  Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dares Salaam.

Aidha Serikali imefafanua kwamba madai ya watumishi hao yanayohusu mishahara mpaka kufikia Oktoba Mosi,mwaka huu,ambao si walimu   malimbikizo yake yalikuwa takribani Sh. bilioni 6.147,  na idadi ya watumishi wanaodai ni 5,695  katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016.

Hivyo hadi kufikia Oktoba , mwaka huu Serikali ilikuwa  imewalipa watumishi 1,551 wakiwemo wa Serikali za Mitaa jumla ya Sh. bilioni 1.6 na malipo hayo  hayajumuishi yale yaliyofanyika kwa walimu.
“Aidha Watumishi  wa Serikali  za Mitaa wapatao  455 wenye madai  ya Sh. milioni 593.2 watalipwa mwezi  Oktoba, mwaka huu. Madai yaliyosalia yataendelea  kulipwa  kila mwezi kadri uhakiki unavyokamilika,” alisema Kaimu Katibu Mkuu huyo.  

Alisema  kwa upande wa madai  yasiyohusu mishahara , ambayo yamekuwa yakilipwa  kupitia fungu la Matumizi  Mengineyo, madai ya kiasi  Sh. bilioni 18 yalikwishahakikiwa na yanasubiri kulipwa.  

Mkwizu aliongeza kwamba  madeni hayo  ya watumishi hao ni yale  yaliyolimbikizwa hadi mwaka  2012/2013.
“ Serikali imepanga kulipa deni hilo lote katika kipindi cha kuanzia Oktoba 2013 hadi Januari,2016,kwa kuanzia Oktoba 2015 Serikali imetenga kiasi cha Sh. bilioni 4 na kiasi cha sh. bilioni 14 kitakachosalia kitalipwa kwa awamu ndani ya kipindi kilichopangwa,” alisisitiza.

Aidha Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema wakati wa kutekeleza malipo hayo, waajiri wameaagizwa kuwaandikia barua watumishi ambao madai yao yamekataliwa au kupunguzwa ili kuwafahamisha sababu za kutakataliwa  kwake na hivyo kuwawezesha kuwa na taarifa sahihi kuhusu madai  yao na kuondoa uwezekano wa kudai mara nyingine.

 Akizungumzia kuhusu suala la uhakiki wa madeni alisema  kwa upande wa madai yasiyohusu mishahara yalikuwa ni sh.  bilioni 18,lakini baada ya kuhakikiwa yakafikia Sh. bilioni 14.

 Alizitaja sababu mbalimbali za kukataliwa  baadhi ya madeni hayo  kuwa ni  zipo tofauti na zinatokana na kutofuata  sheria, kanuni na taratibu.

RATIBA YA KUAGA MWILI WA MHE:DEO FILIKUNJOMBE(MB) MTONI KIJICHI TEMEKE DARE ES SALAAM OKTOBA 17, 2015

WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUWASILI KESHO

0
0
EAST AFRICAN COMMUNITY




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUNDI la waangalizi wa uchaguzi Mkuu nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanatarajia kuwasili Dar es Salaam Jumapili, tarehe 18 October  2015 tayari kwa uangalizi wa uchaguzi kwa upande wa Tanzania Bara na Visiwani.


Kuwasili kwa kundi la Jumuiya ya Afrika Mashariki lenye takribani watu hamsini na tano, ni kuitikia mwaliko kutoka kwa Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kufuata Maazimio ya Baraza la Mawazili la Jumuiya ya Afrika Mashariki juu ya uangalizi wa uchaguzi kwa nchi Wanachama wa Jumuiya.


Kazi ya wasimamizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa ni kuangalia kwa ujumla wake mazingira ya uchaguzi na kutathmini kwa kina mchakato wa uchaguzi nchini kote kabla, kipindi cha uchaguzi na baada ya siku ya uchaguzi.


Kundi la waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki litaongozwa na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kenya, Mh. Awori Arthur Athansius Moody.


Kundi waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki litatangaza uwepowake inchini Tanzania kwenye mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika Jumatatu, tarehe 19, October 2015, saa mbili na dakika thelathini (8.30am) asubui, New Africa Hotel, Dar es Salaam.


·         NINI KITAFANYIKA- Kutoa taarifa ya kuwasili kwa waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki



·         WAPI-New Africa Hotel, Dar es Salaam



·         LINI- Tarehe 19th October 2015 from 8.30 am -10.30am

  
Ndugu   Muandishi wa Habari, unaombwa kuthibitisha uwepo wako kwenye mkutano huu kupitia anuani zifutazo hapa chini;


Owora Richard Othieno,

Press and Protocol Coordinator

EAC Election Observer Mission

New Africa Hotel


Dar es Salaam, Tanzania

Tel: +255 784 835021; 

WAHITIMU WAASWA KUACHANA NA FIKRIA POTOFU KUWA ELIMU WANAYOIPATA ITAWAPATIA AJIRA SERIKALINI AU KWENYE SEKTA BINAFSI

0
0


Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Bwawani.
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Bwawani wakigani shairi lao mbele ya Mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akimkabidhi cheti Mwanafunzi Mhitimu kwenye Mahafali ya Kumi na mbili ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Bwawani Oktoba 16, 2015(kulia kwa Mgeni rasmi) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.


Na Lucas Mboje, Pwani.
WAHITIMU wa kidato cha nne nchini wameaswa kuachana na fikria potofu kuwa elimu wanayoipata itawapatia ajira Serikalini au kwenye Sekta binafsi badala yake watumie elimu hiyo kama nyenzo muhimu ya kuwawezesha kujiajiri wao wenyewe.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil alipokuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya kumi na mbili ya kidato cha nne katika shule ya Bwawani Sekondari iliyopo Mkoani Pwani.

"Katika hali ya sasa ya utandawazi yapo mambo kadhaa ambayo mtu binafsi anaweza kuyafanya na kujipatia kipato cha kujiendeleza maisha yake". Alisema Bw. Abdulwakil.

Bw. Abdulwakil amesisitiza kuwa wanachotakiwa kufanya wahitimu hao ni kuyasoma mazingira ya maisha popote watakapokuwa na kuamua namna ya kujiajiri ili mradi isiwe shughuli zinazopingana na sheria na maadili ya kijamii, kama vile kuuza madawa ya kulevya, ukahaba, unyang'anyi na mambo mengine yanayofanana na hayo.

BONDIA VICENT MBILINYI AMPIGIA MIKWALA DEO NJIKU KUPAMBANA DESEMBA 25

0
0
BONDIA VICENT MBILINYI


Na Mwandishi Wetu

BONDIA Vicent Mbilinyi amesaini mkataba wa kuzipiga na Deo Njiku wa Morogoro siku ya Desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogo wakisindikiza mpambano wa Fransic Cheka na Thomasi Mashali mpambano uho wa raundi sita

utakuwa wa kwanza kwa bondia Mbilinyi kucheza mkoa wa morogoro akizungumzia mpambano huo bondia huyo amesema kuwa anamjua mpinzani wake vizuri kutokana na ukongwe wake kwa kuwa alianza zamani kupigana ata hivyo mimi nina jiamini na nitamkalisha katika raundi za awali

bondia huyo alieweka kambi yake mkoa wa pwani maeneo ya Kibaha ambapo ameweka kambi yake kwa ajili ya mpambano huo
bondia huyo anaefundishwa na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi ncini Rajabu Mhamila 'Super D' amejizatiti kumtwanga vizuri tu Deo njiku ili ajisafishie njia ya kuwa bingwa wa mchezo wa masumbwinchini

nae Kocha wake Rajabu Mhamila 'Super D;' aliongeza kwa kusema kuwa ana matumaini na bondia wake kwa kuwa na rekodi nzuri ya mchezo ambapo mpaka sasa amecheza michezo 7 kashinda 5 droo 1 na kupoteza 1 kwa rekodi hiyo bondia huyo ana uchu wa kubaki kileleni na kuendeleza kichapo kwa kila bondia anaekutana nae

EAC TO COLLABORATE WITH THE NELSON MANDELA AFRICAN INSTITUTION OF SCIENCE AND TECHNOLOGY (NM-AIST) TO ENHANCE THE COMMUNITY’S SCIENCE AND TECHNOLOGY STRATEGY

0
0
Amb. Dr. Richard Sezibera, EAC Secretary General (left), being greeted upon arrival to NM-AIST grounds by the Institution’s Vice Chancellor, Prof. Burton Mwamila.
hhh
Amb. Dr. Richard Sezibera, EAC Secretary General (centre), handing over a gift token of the EAC flag and other publications to NM-AIST’s Vice Chancellor, Prof. Burton Mwamila (second left). Celebrating in this auspicious moment are Aloysius Chebet, EAC Principle Education Officer (second right) and Prof. Lughano Kusiluka (far left), NM-AIST’s Deputy Vice Chancellor responsible for Academic Research and Innovation.
Master’s student in Life Sciences (LiSE), Ms. Winfrida Makirita (second left), explaining to the EAC delegation and other observers, about the benefits of medicinal plants for the treatment of stomach pains and fungus, and as a component for mosquito repellent.
East African Community
 
PRESS RELEASE
EAC TO COLLABORATE WITH THE NELSON MANDELA AFRICAN INSTITUTION OF SCIENCE AND TECHNOLOGY (NM-AIST) TO ENHANCE THE COMMUNITY’S SCIENCE AND TECHNOLOGY STRATEGY

…..Higher learning institutions like NM-AIST are reshaping Africa’s future through top-notch teaching and relevant research.
           
East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania, October 17, 2015: Amb. Dr. Richard Sezibera, Secretary General of the East African Community (EAC) yesterday paid a courtesy visit to the Nelson Mandela African Institution of Science and Technology (NM-AIST) . He was accompanied by Mr. Aloysius Chebet, EAC Principle Education Officer and Ms. Alice Maro, EAC Communications Expert.

At the occasion, Prof. Burton Mwamila, NN-AIST Vice Chancellor, expressed his gratitude to the Secretary General for taking time off his busy schedule to visit to the Institution. After his opening remarks, Prof. Mwamila gave an overview presentation on NM-AIST to the EAC delegates, and some 150 attendees comprising of NM-AIST faculty staff members and students.

During his keynote address Amb. Sezibera commended the Government of the United Republic of Tanzania for investing in the establishment of the Institution.

He further urged leaders of other EAC Partner States to also support NM-AIST, so as to “further develop it into a Regional hub where brilliant and great minds of East African sons and daughters can experiment and transform their innovative ideas into real solutions and products for the economic transformation of the region and the continent at large.”

Further into his speech, the Secretary General talked about alarming numbers of science and engineering graduates in Africa, currently standing at 35 scientists and engineers per million inhabitants. He attributes this low figure to the ever-growing brain drain of the well-educated and skilled populations, as well as to the low GDP spending by African governments on Research and Development (R&D). Only three countries in Africa spend one percent of their GDP on R&D: Uganda, Malawi and South Africa.

The Secretary General was taken on a campus tour of NM-AIST where he visited the laboratory complex to further identify areas of collaboration for the two institutions.
​Note to Editor

About the Nelson Mandela African Institution of Science and Technology (NM-AIST)

NM-AIST, based in Arusha, Tanzania, is in a network of Pan-African Institutions of Science and Technology located across Sub-Saharan Africa (SSA). These Instituions, which are the proud brainchild of the late President Nelson Mandela, envision training and developing the next generation of African scientists and engineers with a view of impacting on the continent’s development through the application of science, engineering and technology (SET).

Accredited by the Tanzania Commission for Universities (TCU), NM-AIST currently offers eight Master’s and PhD Programmes in Life Sciences (LiSE); Bio-engineering (BioE); Mathematical and Computer Science and Engineering (MCSE); Information and Communication Science and Engineering (ICSE); Materials Science and Engineering (MaSE); Hydrology and Water Resources Engineering (HWRE); Environmental Science and Engineering (EnSE) and Sustainable Energy Science and Engineering (SESE).


For more information please contact: Owora Richard Othieno, Head of Department; Corporate Communications and Public Affairs; Tel: +255 784 835021; Email: othieno@eachq.org

MAMIA WAMUAGA MBUNGE WA LUDEWA DEO FILIKUNJOMBE NA NDUGU ZAKE NYUMBANI KWAKE KIJICHI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe enzi za Uhai wake.
 Msaidizi wa Mbunge huyo, Casablanga Haule enzi za Uhai wake.
 Padri Plasdus Ngabuma enzi za Uhai wake.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe wakati wa ibada ya kuuaga iliyofanyika nyumbani kwake Kijichi Dar es Salaam leo mchana.
 Majeneza yenye miili ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe na ndugu zake, Plasdus Ngabuma na Casablanga Haule yakiwa yamewekwa mbele wakati wa ibada ya kuiombea iliyofanyika nyumbani kwa mbunge huyo Kijichi Dar es Salaam leo, kabla ya kusafirishwa kwenda Ludewa kwa mazishi.
 Mjane wa Deo Filikunjombe, Sarah (katikati) akisaidiwa na jamaa zake wakati wa ibada hiyo.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

PINDA AAGWA NA WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU

0
0


  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda kizungumza katika hafla fupi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kumuaga Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda iliyofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijjni Dar es salaam Oktoba 16, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakigonganisha glass na Watendaji wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika Hafla fupi ya kumuaga aliyoandaliwana  watumishi wa Ofisi yake kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Oktoba 16, 2015.   Wapili kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka, kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Regina Kikuli  na wapili kulia ni Msajili wa Vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MABONDIA YONAS SEGU NA IDI PIALALI WAPIMA KUZITO KUZIPIGA KESHO JUMAPILI

0
0


Mratibu wa mpambano wa masumbwi Antony Rutta Katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Yonas Segu kushoto na Idi Pialali kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili hii katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam Picha na SUPERD BOXING NEWS

Bondia Yonas Segu kushoto akitunishiana misuli na Idi Pialali mara baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kesho jumapili utakaofanyika katika ukumbi wa Frends corner Manzese Dar es salaam Picha na SUPERD BOXING NEWS
Bondia Ismail Ndende kushoto akitambiana na Mwinyi Mzengela baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho jumapili Picha na SUPERD BOXING NEWS

RAIS KIKWETE AAGANA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE

0
0

Balozi wa Tanzania Afrika ya Kusini Radhia Msuya na Balozi wa Tanzania nchini India Alan Kijazi wakimkabidhi zawadi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa niaba ya mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje wakati wa hafla ya kutunuku tuzo kwa Mhe.Rais  iliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre(JNICC) jijini Dar es Salaam leo.  
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre(JNICC) jijini Dar es Salaam leo.
(picha na Freddy Maro) 

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WAKIRI WAZI HAIJAPATA KUTOKEA,WAELEZA HISIA ZAO KUWA MAGUFULI ANATOSHA NAFASI YA URAIS.

0
0
 Dkt. Magufuli (katikati) akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Nyamagana (pichani kulia) Ndugu Stanslaus Mabula mbele ya Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo.Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza waliohojiwa na Globu ya Jamii walieleza na kukiri wazi kuwa haijawahi kutokea kwa mapokezi haya makubwa na ya aina yake,na kuwa Magufuli ndiye anaetosha kuvaa viatu vya Urais.
 Dk Magufuli (katikati) akiwanadi Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela, Anjela Mabula 
 Dk Magufuli (katikati) akiwanadi Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela, Anjela Mabula na Stanslaus Mabula ambaye anagombea ubunge Jimbo la Nyamagana.
 Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika mithili ya Utitiri kwenye uwanja wa Furahisha jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na kuwaomba wampigie kura za kutosha ifikakapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia  Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo jijini Mwanza kwenye mkutano wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na kuwaomba wampigie kura za kutosha ifika Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa jiji la Mwanza wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akizinadi sera zake. 
 sehemu ya umati wa watu ndani ya viwanja vya furaisha jijini Mwanza jioni ya leo.

 Wananchi wakiuzuia msafara wa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Pombe Magufuli  uliokuwa ukisindikizwa na umati wa watu kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwenda kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

 Wananchi wa Jiji la Mwanza wakiwa wametandika vitenge kwenye lami ili msafara wa Dk Magufuli upite kuelekea kwenye mkutano wa Kampeni katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo jijini Mwanza.
 Mgombea urai wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza
 Mgombea urai wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiwaaga baada ya mkutano wa kampeni kumalizika katika viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza
 Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John pombe Magufuli ukiondoka katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo mara baada kumaliza mkutano wa kampeni,huku ukisindikizwa na umati mkubwa wa watu.

PICHA NA MICHUZI JR-JIJINI MWANZA.


WANANCHI WAMETAKIWA KULINDA AMANI SIKU YA UCHAGUZI MKUU-MAKONDA

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
IKIWA  zimebakia siku nane kufikia Uchaguzi Mkuu, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda  amewataka wananchi wa wilaya hiyo kusimamia amani na utulivu wa nchi  bila kufanya hivyo  ahadi za wagombea wote hazitoweza kutekelezeka na badala yake kuanza kuugua maumivu ya uchaguzi huo

Makonda ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni pamoja na wenyeviti  wa serikali za mitaa, wagombea wa ngazi mbalimbali za uongozi, wasimamizi wa uchaguzi na viongozi wa vyama vya siasa .

“ Sisi sote tunatoka katika itikadi tofauti tofauti lakini wote tupiganie maendeleo yaTaifa kwa ujumla kuweza kupiga kura kwa staha kuweza kulinda amani na vikundi vyovyote visiweze kukaa katika eneo la kupigi kura" amesema Makonda.

Amesema Wilaya ya Kinondoni isiwe chanzo cha kusambaza chuki na kwamba kila mwenyekiti wa serikali ya mtaa ajitambue kuwa ana mamlaka tosha yakusimamia na kutekeleza uwepo wa amani.

Makonda amesema viongozi wa mitaa wao ndio wenye mamlaka tosha ya kuhakikisha maeneo wanaoishi yanabakia kuwa na amani wakati wa upigaji kura na wakati wa kusubiria matokeo.

Amesema yapo baadhi ya maeneo ambayo watumishi wa serikali wanashindwa kutekeleza wajibu wao ili kuibua chuki kwa wananchi kuwa serikali haiwajibiki kwao, hivyo viongozi wa mitaa watakapooona hali kama hizo wawajibuike kutoa taarifa.

Aidha  Makonda amepiga marufuku  vikundi vinavyoundwa  kwa ajili ya kusimamia kura na kwamba pindi akipata taarifa atawashughulika nao bila aibu katika kuweza  kumalizika kwa uchaguzi huku amani ikitawala.

Nae Mkurugenzi wa Kinondoni, Mussa Natty amesema suala la ulinzi na usalama  ni la kila mtu  na  kuwataka viongozi wa mitaa kutoa taarifa ya kile kinachofanyika katika maeneo yao.


Amesema wananchi wanatakiwa kukaa mita 200 baada ya kupiga kura, na kama kuna kijiwe ambacho kina wakereketwa wasiwepo  katika eneo hilo ni amri.

DKT MAGUFULI ASHIRIKI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU DEO FILIKUNJOMBE NA WENZAKE WAWILI WALIOFARIKA KATIKA AJALI YA HELIKOPTA..

0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli  akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.PICHA NA MICHUZI JR.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimfariji Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe akilia kwa uchungu kufuatia kifo cha Mumewe Deo Filikunjombe,wakati wa kuaga katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 Dkt Magufuli akifarijiana na Mh.Zitto Kabwe  wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 Dkt Magufuli alishindwa kujizuia kutoa machozi ya huzuni  wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 Majeneza yenye miili ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe na ndugu zake, Plasdus Ngabuma na Casablanga Haule yakiwa yamewekwa mbele ya waombolezaji  wakati wa kuaga katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. kabla ya kusafirishwa kwenda Ludewa kwa mazishi mkoani Njombe.

UWANJA WA FURAHISHA HAUTOSHI KWA DKT MAGUFULI

MAGUFULI ALIVYOUNGURUMA VIWANJA VYA FURAHISHA JIJINI MWANZA

TAMASHA LA KANDANDA DAY LAFANYIKA LEO JJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Mgeni rasmi  Angetile Osiah akizugumza katika  Tamasha la Kandanda Day 2015, hufanyika kila mwaka mwezi oktoba kwa kuzikutanisha Team Ismail  (Blue Jersey)na Dizo Moja (White Jersey) lilofanyika katika viwanja vya TCC Sigara, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Bin Slum Tyres, Nassor Binslum, akionesha makeke yake uwanjani wakati wa Tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa timu  Ismail wakionyesha furaha ya ushindi Tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi  Angetile Osiah akiwa na wanakamati wa timu katika picha ya pamoja katika  Tamasha la Kandanda Day 2015, Lilofanyika katika viwanja vya TCC Sigara, leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images